Posts

Ujue Ugonjwa Wa PID BY DR CHRISS

  Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (vagina) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari. Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote. Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno. Dalili Za PID PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa: . Maumivu – yanayoweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga . Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya . Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi . Maumivu wakati wa kujamiiana . Homa, wakati mwingine kusikia baridi . Maumivu wakati wa h...

vidonda vya tumbo

*Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya* kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo. Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, homa, kupungua uzito. CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni; 1.Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori) 2.Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zing...

Ujue Ugonjwa Wa PID

  Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (vagina) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari. Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote. Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno. Dalili Za PID PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa: . Maumivu – yanayoweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga . Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya . Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi . Maumivu wakati wa kujamiiana . Homa, wakati mwingine kusikia baridi . Maumivu wakati wa h...

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUSAINI MKATABA WA AJIRA" 💼✍️

Ukiwa na furaha kubwa kwa kupata mkataba wa ajira na mwajiri wako mpya! 💼✨ Ni muhimu kufuata hatua hizi muhimu kabla ya kusaini: 1️⃣ SOMA KWA MAKINI: Hakikisha kusoma kila kifungu cha mkataba wako. Elewa masuala ya mshahara, majukumu, likizo, na masuala mengine ya kisheria. Kama kuna maswali, wasiliana na mwajiri wako ili upate ufafanuzi.  2️⃣ PATA USHAURI WA KITAALUMA: Ili kuepuka shida zisizotarajiwa, ni busara kupata ushauri kutoka kwa wakili, mshauri wa masuala ya ajira. Watakusaidia kuelewa masuala ya kisheria na haki zako kama mfanyakazi.  3️⃣ JADILIANA KWA HESHIMA: Ikiwa una wasiwasi kuhusu baadhi ya vifungu, muulize mwajiri wako kwa heshima. Kumbuka, mazungumzo ni sehemu ya mchakato wa ajira na haimaanishi unaonyesha kukataa mkataba.   4️⃣ WEKA KUMBUKUMBU: Hifadhi nakala ya mkataba wako na mawasiliano yote na mwajiri. Hii itakuwa muhimu ikiwa kutatokea mabishano au mizozo baadaye.   5️⃣ ZINGATIA MUDA: Fanya uamuzi kabla ya muda wa mwisho wa kusaini mkataba. ...

*MOYO KUPANUKA SIO TATIZO LINALOSABABISHWA NA MOYO WENYEWE

Moyo kupanuka au kuwa mkubwa ni tatizo ambalo huathiri utendaji wa mfumo wa usambazaji damu mwilini. Ni hali inayosababishwa na ukinzani wa moyo jinsi unavyotoa na kuingiza damu katika mishipa ya moyo na kuelekea sehemu mbalimbali za mwili. Moyo kupanuka kutokana na mazingira ya kusukuma damu kwa nguvu ya ziada tofauti na kawaida, hivyo kusababisha misuli ya moyo kuharibika. Wakati mwingine moyo hutanuka bila sababu zinazojulikana moja kwa moja. Pia, wakati mwingine moyo unaweza kutanuka kwa kipindi kifupi kutokana na mgandamizo kwenye mwili wako mfano ujauzito. Hali nyingine ni tatizo la moyo ulilozaliwa nalo, kuharibika kwa moyo kutokana na mshtuko wa moyo, kudhoofu kwa misuli ya moyo au moyo kutodunda kwa mpangilio. Mazingira hayo huweza kusababisha moyo kutanuka. Hali zingine za kiafya zinazohusiana na moyo kutanuka ni kama zifuatazo: Kupanda kwa shinikizo la damu Hali hii husababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu zaidi ili kuifikisha sehemu mbalimbali za mwili. Hali inayosababisha ...

*TAMBUA VIPIMO VINAVYOHUSIKA KUPIMA TEZIDUME ILI KUBAINI TATIZO*

Njia ziko nyingi daktari wako ataamua atumie njia gani kutokana na hatua ya tatizo lako  lilivyo. Hizi ni baadhi ya njia;👇 1..KUCHUNGUZA TEZI DUME KUPITIA NJIA YA HAJA KUBWA AU DIGITAL RECTAL EXAMINATION (DRE) upimaji tezi dume Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini. 2.KIPIMO CHA DAMU CHA PROSTATE-SPECIFIC ANTIGEN (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume. 3.UTRASOUND YA PURU (RECTAL ULTRASOUND) Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa...

ZIJUE SABABU ZA MIMBA KUTOKA KABLA YA WAKATI

➡️Mimba kuharibika au miscarriage ni kitendo cha kupoteza kichanga kwa mama mjamzito kabla ya muda wa kujifungua kuwadia.     Mara nyingi hutokea ndani ya miezi mitatu ya mwanzo baada ya kushika ujauzito. sababu za  mimba kutoka zinatofautiana kwa kila mwanamke. ➡️ Namna 5 za Mimba Kuharibika na Kutoka.    ➡️ Kuna aina namna nyingi za mimba kuharibika. Kwa Kutegemeana na sababu ya mimba yako kutoka mapema pamoja na hatua ya ukuaji wa mimba aina hizi zinaweza kuainishwa kama ifuatavyo 1️⃣  Blighted ovum: ni pale yai lililorutubishwa linajipandikiza kwenye ukuta wa uterus lakini mimba haikui na kupelekea kuharibika. 2️⃣  Complete miscarriage: ni pale kiumbe kilichotungwa kinatolewa nje ya mfuko wa mimba. Inaweza kusababisha damu kuvuja 3️⃣ Missed miscarriage: Ni pale kiumbe kidogo kufariki tumboni pasipo kupata viashiria vyovyote 4️⃣ Reccurent miscarriage: ni pale mimba zako zinapotoka mfululizo mara 3 au zaidi ndani ya miei mitatu ya kwanza 5️⃣Threatene...