vidonda vya tumbo
*Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya* kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.
Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, homa, kupungua uzito.
CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;
1.Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
2.Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
3.Kuwa na mawazo mengi
4.Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
5.Kunywa pombe na vinywaji vikali
6.Uvutaji wa sigara
7.Kuto kula mlo kwa mpangilio
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili kama;
1.Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
2.Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo
3.Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
4.Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
5.Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
6.Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
7.Kushindwa kupumua vizuri
JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO
1.Kunywa maji mengi
2.Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo
3.Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)
4.Usivute sigara
5.Punguza au acha kunywa pombe
6.Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
7.Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9
TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO.
Watu wengi wamekuwa hawaponi vidonda vya tumbo au wakipona hawamalizi mda mrefu tatizo linarudi tena KWA nini?
Hii ni kutokana na dawa nyingi kukosa zink ambayo huweza kukausha vidonda na kukuimarisha zaidi.
Comments