*TAMBUA VIPIMO VINAVYOHUSIKA KUPIMA TEZIDUME ILI KUBAINI TATIZO*


Njia ziko nyingi daktari wako ataamua atumie njia gani kutokana na hatua ya tatizo lako  lilivyo.

Hizi ni baadhi ya njia;👇

1..KUCHUNGUZA TEZI DUME KUPITIA NJIA YA HAJA KUBWA AU DIGITAL RECTAL EXAMINATION (DRE)

upimaji tezi dume
Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.

2.KIPIMO CHA DAMU CHA PROSTATE-SPECIFIC ANTIGEN (PSA):
PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.

3.UTRASOUND YA PURU (RECTAL ULTRASOUND)
Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.

4.KIWANGO CHA UTOKAJI WA MKOJO (URINE FLOW STUDY):
Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.

5.KIPIMO CHA KUCHUNGUZA KIBOFU CHA MKOJO (CYSTOSCOPY):
Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.

Matibabu ya Tezi Dume.
Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

Matibabu kwa Njia ya Dawa
Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake.

Matibabu kwa Njia ya Upasuaji
Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo niTiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume.

Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Tiba ya kutumia Joto la maji (Water-induced thermotherapy):
Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume. Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH.

Aina Za Upasuaji wa Tezi dume
Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).

Madhara Ya Upasuaji
Kukosa uwezo wa kufikia kishindo yani hutoi shahawa(retrogade ejaculation) wazee wengi hulalamika sana baada ya hizi operation hivyo ushauri nasaha lazima utolewe ili mgonjwa ajue nini madhara yake kabla ya operation.
Kuziba kwa njia ya mkojo kutoka na kuumia kwa njia hizo wakati wa kitendo hicho. Baadaya ya upasuaji mgonjwa anapoendelea kupona kovu linaweza kuziba njia ya mkojo.
Shida ya kushindwa kudhibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kudhibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.
Kutokwa na damu katika siku za awali mara baada ya upasuaji kupitia njia ya mkojo: Kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo.
Wanaume kuwa wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuaji wa tezi dume huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.

*Kama una maswali au maelezo zaidi tumia namba hii 254115454237*

Comments

Popular posts from this blog

Ujue Ugonjwa Wa PID BY DR CHRISS

ATHARI ZA KUSUKA, KUWEKA DAWA KWA KINA DADA*

ZIJUE SABABU ZA MIMBA KUTOKA KABLA YA WAKATI