Posts

Showing posts with the label NGOKO ☝️

*MOYO KUPANUKA SIO TATIZO LINALOSABABISHWA NA MOYO WENYEWE

Moyo kupanuka au kuwa mkubwa ni tatizo ambalo huathiri utendaji wa mfumo wa usambazaji damu mwilini. Ni hali inayosababishwa na ukinzani wa moyo jinsi unavyotoa na kuingiza damu katika mishipa ya moyo na kuelekea sehemu mbalimbali za mwili. Moyo kupanuka kutokana na mazingira ya kusukuma damu kwa nguvu ya ziada tofauti na kawaida, hivyo kusababisha misuli ya moyo kuharibika. Wakati mwingine moyo hutanuka bila sababu zinazojulikana moja kwa moja. Pia, wakati mwingine moyo unaweza kutanuka kwa kipindi kifupi kutokana na mgandamizo kwenye mwili wako mfano ujauzito. Hali nyingine ni tatizo la moyo ulilozaliwa nalo, kuharibika kwa moyo kutokana na mshtuko wa moyo, kudhoofu kwa misuli ya moyo au moyo kutodunda kwa mpangilio. Mazingira hayo huweza kusababisha moyo kutanuka. Hali zingine za kiafya zinazohusiana na moyo kutanuka ni kama zifuatazo: Kupanda kwa shinikizo la damu Hali hii husababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu zaidi ili kuifikisha sehemu mbalimbali za mwili. Hali inayosababisha ...

*TAMBUA VIPIMO VINAVYOHUSIKA KUPIMA TEZIDUME ILI KUBAINI TATIZO*

Njia ziko nyingi daktari wako ataamua atumie njia gani kutokana na hatua ya tatizo lako  lilivyo. Hizi ni baadhi ya njia;👇 1..KUCHUNGUZA TEZI DUME KUPITIA NJIA YA HAJA KUBWA AU DIGITAL RECTAL EXAMINATION (DRE) upimaji tezi dume Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini. 2.KIPIMO CHA DAMU CHA PROSTATE-SPECIFIC ANTIGEN (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume. 3.UTRASOUND YA PURU (RECTAL ULTRASOUND) Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa...

seventh Adventist day church logo

Image
Exodus 20:8

FAIDA 48 ZA JUISI YA TANGAWIZI AMBAZO ULIKUWA HUZIJUWI

  1. Huondoa sumu mwilini haraka sana 2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi 3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi 4. Huondoa uvimbe mwilini 5. Huondoa msongamano mapafuni 6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake 7. Huondoa maumivu ya koo 8. Huua virusi wa homa 9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini 10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills) 11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya. 12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol” 13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-r elated cancer) 14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia) 15. Ni ...

ATHARI ZA KUSUKA, KUWEKA DAWA KWA KINA DADA*

Image
✅NI dhahiri kwamba kati ya wanawake kumi, mmoja tu ndiye unayeweza kumkuta akiwa na nywele zake za asili, waliosalia  utawakuta aidha wamesuka, wameshonea nywele za bandia (weaving) au wameweka dawa. ✅Wengi hufanya hivyo kwa sababu ya kusaka urembo na kupendezesha muonekano wao. ✅Utafiti uliofanywa na wataalamu wa kliniki ya Cleveland iliyoko nchini Marekani, umebaini kuwa wanawake wanaobadili nywele zao wako katika hatari ya kupoteza nywele zao za asili. ✅Watafiti hao wanaeleza katika matokeo ya utafiti wao uliowahusisha wanawake 326 wenye asili ya Kiafrika (African-American) ambao baadae ulichapishwa katika jarida la ‘Archives of Dermatology’. ✅Wanaeleza kwamba mwanamke anayesuka mara kwa mara hujiweka kwenye hatari zaidi ya kunyonyoka nywele zake za asili ikilinganishwa na yule anayesuka mara chache. ✅Kwamba, urembo huo uchangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha maambukizi kwa kuzaliwa bakteria ambao uharibu mfumo mzima wa ukuaji wa nywele na kuharibu ute ute mu...