zijue silaha 5 katika ulimwengu wa roho
Nawasalimu wote wanajukwaa,leo nataka tujifunze silaha kuu tano zinazotumika katika ulimwengu wa kiroho. Kama wengi tunavyojua kuwa katika ulimwengu wa kiroho kuna falme kuu mbili,falme ya kwanza ni ufalme wa nuru na falme ya pili ni ufalme wa giza. Falme zote hizi zina muundo na uongozi na mamlaka kamili.Katika viumbe vyote binadamu ndiyo kiumbe pekee mwenye sifa ya kuweza kuishi katika ulimwengu wa kiroho na ulimwengu huu wa kimwili kwa wakati mmoja.Inawezekana umesoma vitabu vingi sana na kufanya jitihada nyingi sana ili ufanikiwe katika maisha yako lakini bado umeshindwa. Nakushauri fuatilia darasa hili kwa umakini na siku ukimaliza Lazima ufanikiwe kwa kuwa manbo yote huanzia katika ulimwengu wa kiroho na ndicho utakachojifunza hapa. Zifuatazo ni silaha kuu tano za ulimwengu wa kiroho. 1. Damu 2. Jina 3. Kiti 4. Maneno 5. Ardhi na Mbingu Ukiweza kujifunza silaha hizi kwa umakini,utaweza kujua ulimwengu wa kiroho unavyofanya kazi,utapata nguvu za kuingia katika ulimwengu...