Ujue Ugonjwa Wa PID
Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (vagina) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari. Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote. Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno. Dalili Za PID PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa: . Maumivu – yanayoweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga . Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya . Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi . Maumivu wakati wa kujamiiana . Homa, wakati mwingine kusikia baridi . Maumivu wakati wa h...